SOKA: Simba SC yasema Manula yupo salama
2021-03-03 15:39:19| cri

Hali ya kiafya ya Mlinda Mlango chaguo la kwanza la Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Aishi Salum Manula imeendelea kuimarika baada ya kupata matibabu kwenye Hospitali ya Kairuki, jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba SC, kupitia ukurasa wao wa Instagram, Manula aliumia Jumatatu akiwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Haji Manara ametoa taarifa za kuendelea vyema kwa Mlinda Mlango huyo sanjari na kuruhusiwa kutoka hospitali mapema jana.