SOKA: Guardiola atamba lakini atoa tahadhari
2021-03-04 16:00:28| cri

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema anajivunia kiwango bora cha timu yake lakini amekitahadharisha kikosi chake kuwa wanahitaji kuendelea kupata matokeo mazuri ili wakusanye alama nyingi zaidi na kumpora ubingwa, bingwa mtetezi klabu ya Liverpool. Guardiola ameyasema hayo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Wolverhampton kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza uliochezwa jumanne usiku kwenye uwanja wa nyumbani wa Manchester City, Etihad. Baada ya ushindi huo, Manchester City wameweka rekodi ya kuwa timu pekee kupata ushindi kwenye michezo 15 mfululizo ya EPL msimu huu, huku ikifikisha ushindi wake wa michezo 21 mfululizo kwenye michuano yote.