Watu 10 wafariki kwenye ajali ya kuanguka kwa ndege nchini Sudan Kusini
2021-03-04 09:23:37| cri

 

 

Mkuu wa jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini amethibitisha kuwa, ajali ya kuanguka kwa ndege iliyotokea tarehe 2 jioni jimboni humo imesababisha vifo vya watu 10 wakiwemo marubani wawili.

Imefahamika kuwa ndege hiyo ya kibiashara ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa jimbo la Jonglei, na chanzo cha ajali hiyobado hakijajulikana.

Tangu mwaka 2015, ajali nyingi za kuanguka kwa ndege zimekuwa zikitokea nchini Sudan Kusini, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.