Wagombea zaidi ya 2,000 wajiandikisha kugombea nafasi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Ethiopia
2021-03-04 08:35:10| CRI

Tume ya Uchaguzi ya Ethiopia (NEBE) imesema wagombea zaidi ya elfu mbili kutoka vyama 15 vya kisiasa wamejiandikisha kugombea nafasi kwenye uchaguzi mkuu wa sita wa Ethiopia, ulioahirishwa kufanyika kutoka Agosti 29 mwaka 2020, kutokana na janga la virusi vya Corona.

Uchaguzi wa mwaka huu utafuatiliwa kwa karibu na waangalizi wa ndani na wa kigeni, ambapo chama tawala kilichobadilisha jina kuwa Chama cha Ustawi (PP), kitakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa vyama vya upinzani.