Msaada wa chanjo ya COVID-19 wa China kwa Guinea wawasili Conakry
2021-03-04 09:27:01| CRI

Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa kama msaada na China kwa Guinea iliwasili jana huko Conakry. Waziri wa mambo ya nje wa Guinea Bw. Ibrahima Kaba, waziri wa afya Bw. Colonel Rémy Lamah na balozi wa China nchini Guinea Bw. Huang Wei walihudhuria hafla ya kukabidhi chanjo hiyo kwenye uwanja wa ndege.

Akiongea kwenye hafla hiyo, Bw. Kaba ameishukuru serikali ya China na watu wake, na kusema baada ya kutoa ombi la msaada kwa China, China ilijibu mara moja na kutoa misaada kwa wakati. Amesema msaada huo wa China umeipatia serikali ya Guinea mbinu yenye ufanisi ya kulinda afya ya wananchi wake, na anaamini kuwa Guinea hakika italishinda janga la COVID-19 chini ya uungaji mkono wa China.