KQ kurejesha safari za moja kwa moja kwenda Paris,Ufaransa
2021-03-04 19:07:29| cri

Shirika la Ndege la Kenya Airways , KQ, limetangaza mipango ya kurejesha safari za moja kwa moja kutoka Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi hadi uwanja wa Charles De Gaulle (CDG),jijini Paris, nchini Ufaransa.

Ndege hizo za moja kwa moja zinatarajiwa kuanza tarehe 17 Machi 2021.

Shirika hilo limesema litaendelea kuwapa wateja wake nauli za bei nafuu na uunganishaji wa kituo kimoja kupitia kitovu chake jijini Nairobi hadi sehemu nyingine za Kenya na Afrika ikiwa ni pamoja na Kinshasa,Moroni, , Entebbe, Johannesburg, na Antananarivo.

Shirika hilo le ndege litaanza na ndege moja kwa wiki huku idadi ya safari ikiongezeka kulingana na mahitaji.

Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja wa Shirika la Kenya Airways ,Julius Thairu amesema urejeaji wa safari za moja kwa moja hadi Paris ,Ufaransa ni kwa mujibu wa mipango yao ya kupanua safari zao wakati vikwazo vya usafiri vimeondolewa sehemu nyingi duniani.