Uturuki yatangaza kiwango cha ufanisi cha chanjo ya kampuni ya SINOVAC ya China ni asilimia 83.5
2021-03-04 09:23:03| cri

 

 

Waziri wa afya wa Uturuki amesema kutokana na matokeo ya majaribio ya kimatibabu ya awamu ya tatu yaliyofanywa na kampuni ya SINOVAC ya China nchini Uturuki, kiwango cha ufanisi cha chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na kampuni hiyo ni asilimia 83.5, huku kiwango cha ufanisi wa kukinga maambukizi makali kikiwa ni asilimia 100.

Watu 10,216 waliojitolea walishiriki kwenye majaribio ya kimatibabu ya awamu ya tatu ya kampuni ya SINOVAC yaliyoanza Septemba 14 mwaka jana nchini Uturuki, na hakukuwa na kifo kwenye majaribio hayo.