Watu wanane wachomwa kisu kwenye shambulizi mjini Vetlanda, Sweden
2021-03-04 08:36:17| CRI

Watu wasiopungua wanane wamejeruhiwa baada ya kuchomwa kisu kwenye shambulizi linaloshukiwa kuwa la kigaidi lililotokea jana mjini Vetlanda, kusini mwa Sweden.

Polisi nchini Sweden wamesema, kijana mwenye umri wa miaka 20 aliwashambulia watu wengi kwa kutumia “kitu chenye ncha kali” kwenye maeneo matano tofauti, na baadhi ya wahanga wamejeruhiwa vibaya.

Polisi wameanza uchunguzi ili kujua sababu na lengo la mtuhumiwa huyo kufanya shambulizi hilo.