Chombo cha anga ya juu cha China Tianwen-1 kutua kwenye sayari ya Mars mwezi Mei au Juni
2021-03-04 18:36:58| cri

Chombo cha anga ya juu cha China Tianwen-1 kutua kwenye sayari ya Mars mwezi Mei au Juni_fororder_6159252dd42a2834dd310643195deae217cebfd7

Chombo cha anga ya juu cha China, Tianwen-1 kinasafiri kwa kasi ya kilomita 4.8 kwa sekunde katika mzunguko wa sayari ya Mars, na kinatarajiwa kutua katika sayari hiyo mwezi Mei au Juni mwaka huu.

Mkurugenzi wa Kamati ya Sayansi na Teknolojia iliyo chini ya Shirikisho la Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu, Bao Weimin amesema, chombo hicho kimetuma picha za kwanza za ubora wa juu za Mars.

Amesema chombo hicho kitachunguza mandhari ya sehemu iliyochaguliwa ya kutua na kufuatilia hali ya hewa katika njia za safari ili kukwepa vumbi wakati kikitua kwenye sayari ya Mars.