Uchumi wa Afrika washuka kwa mara ya kwanza katika miaka 25 iliyopita
2021-03-04 18:22:47| CRI

Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni imetoa ripoti ikisema, kutokana na janga la COVID-19, uchumi wa bara la Afrika unashuka kwa mara ya kwanza katika miaka 25 iliyopita.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, janga la COVID-19 limesababisha hasara ya uchumi ya dola za kimarekani bilioni 99 katika bara la Afrika, pia mabadiliko ya tabianchi yameleta athari mbaya kwa uchumi wa Afrika.

Ripoti hiyo imefafanua mkakati wa kufufua uchumi wa Afrika baada ya janga la COVID-19, na kuzitaka nchi mbalimbali za Afrika kutumia nishati safi badala ya mafuta.