Wakulima wa kahawa wa Kenya wapata mapato makubwa zaidi mwaka 2020 licha ya athari za janga la COVID-19
2021-03-04 08:35:49| CRI

Takwimu mpya zilizotolewa jana na Idara ya Taifa ya Takwimu ya Kenya KNBS, zinaonesha kuwa wakulima wa kahawa nchini humo walipata mapato makubwa zaidi mwaka jana kutokana na kupanda kwa bei kwenye soko la kimataifa, licha ya changamoto za janga la virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, thamani ya mauzo ya nje ya kahawa ya Kenya kwenye kipindi hiki yaliongezeka kwa asilimia 9.5 na kufikia dola za kimarekani milioni 202.2, huku kiasi cha mauzo hayo kikishuka kwa asilimia 11 hadi tani 43,483.