Mkutano wa Nne wa Kamati Kuu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa
2021-03-04 18:03:49| cri

Mkutano wa Nne wa Kamati Kuu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa_fororder_1614851571757_329

Mkutano wa Nne wa Kamati Kuu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China umeanza leo mjini Beijing, na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na wa serikali. Wajumbe zaidi ya 2,100 wa Baraza hilo watajadili masuala ya kisiasa na kufikia maafikiano kuhusu utungaji na utekelezaji wa “Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano”.

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lilianzishwa wakati China mpya ilipoasisiwa, na linachukua nafasi kubwa katika utaratibu wa usimamizi wa mambo ya taifa. Baraza hilo linaonesha kazi maalumu katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala muhimu ya siasa, uchumi, utamaduni na maisha ya jamii kupitia majadiliano ya kisiasa, usimamizi wa kidemokrasia, kushiriki na kujadili mambo ya kisiasa, pia ni njia muhimu ya kuonesha demokrasia ya kijamaa.

Mwaka jana ulikuwa mwaka usio kawaida katika historia. Licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, haswa janga la COVID-19, maendeleo ya uchumi na jamii ya China yalipata mafanikio makubwa. Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Wang Yang ameeleza kuwa, baraza hilo lilitekeleza majukumu kwa makini, na kutumia kwa njia zenye ufanisi kufanya majadiliano, ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali unaendelea kwa utaratibu chini ya hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi. Anasema:

“Baraza hili liliandaa shughuli muhimu 23 na kukagua miradi 80 katika mwaka uliopita, na kufanya utafiti na majadiliano kuhusu Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano kwa njia ya kuandaa makongamano, semina kupitia video na mikutano ya utafiti.”

Huu ni mwaka wa 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China, pia ni mwaka wa kwanza kwa China kuzindua mchakato mpya wa kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa. Bw. Wang Yang amesema, baraza hilo litazingatia kazi kuu mbili za mshikamano na demokrasia, kushughulikia vizuri kazi ya utoaji wa mapendekezo na kufikia makubaliano kwa mujibu wa mwongozo na maamuzi ya kamati kuu ya chama, ili kukusanya busara na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Anasema:

“Baraza hili litajadili masuala kuhusu utekelezaji wa mikakati ya kuendeleza vijiji, kukabiliana na tatizo la kuongezeka kwa idadi ya wazee, kuhimiza kazi ya utoaji wa nafasi za ajira kwa njia mbalimbali katika sehemu zenye makabila madogo, kutoa mapendekezo kuhusu masuala muhimu ikiwemo kuanzisha mtandao wa ulinzi wa afya ya umma ya kitaifa, na kutunga mpango kuhusu kazi ya usimamizi wa kidemokrasia, haswa juu ya masuala muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano.”