RIADHA: Rais wa riadha duniani aishauri Tanzania
2021-03-04 16:01:16| cri

Rais wa SHirikisho la Riadha Duniani (WA) Sebastian Coe amesema, anatamani kuona Tanzania ikiwa na Jumba la Makumbusho la Wanamichezo. Coe, mwanariadha nyota wa zamani amesema, ingekuwa na jumba hilo ili kuwakumbuka wanamichezo mahiri walioiletea sifa na heshima nchi hiyo. Coe amesema hayo katika barua yake ya mwaliko kwa Kamati ya Riadha Tanzania (TOC) kuhudhuria uzinduzi wa Makumbusho ya Dunia ya Riadha yatakayofanyika tarehe 11 mwezi huu mjini Monaco, Ufaransa. Amesema uzinduzi wa jumba hilo utawahusisha wanariadha bingwa wa mashindano ya dunia na Olimpiki, akiwemo Filbert Bayi, mwanariadha wa Tanzania aliyevunja rekodi mbili za dunia.