Rais Mwinyi atoa wito kwa Indonesia kuwekeza Zanzibar
2021-03-04 19:08:44| cri

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi,ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Indonesia kuwekeza Zanzibar huku akisema kuwa kuna mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na serikali yake.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana kwenye kikao na Balozi wa Indonesia nchini humo, Prof. Ratlan Pardede alipofika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha.

Dk. Mwinyi alisema Serikali ya Zanzibar imedhamiria kuimarisha uchumi wake, hivyo iko tayari kushirikiana na washirika wengine wa maendeleo ikiwamo Indonesia.

Aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu na Indonesia hasa katika uimarishaji wa sekta mbalimbali za maendelo, hivyo, Serikali anayoiongoza imeacha milango yake wazi kwa wawekezaji wa Indonesia kwenda kuekeza Zanzibar.