Watu milioni 3.8 katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia wapokea msaada wa kibinadamu
2021-03-04 16:33:50| cri

Serikali ya Ethiopia imesema, watu milioni 3.8 katika mkoa wa Tigray, kaskazini mwa nchi hiyo wamepelekewa msaada wa kibinadamu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo imesema, serikali ya Ethiopia imetumia dola za kimarekani milioni 47 kutoa msaada wa chakula na usio wa chakula pamoja na huduma nyingine muhimu katika mkoa huo.

Serikali ya Ethiopia iliruhusu kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu mkoani Tigray wiki iliyopita, na kusisitiza kuwa, mashirika yanayofanya shughuli hizo katika mkoa huo yanapaswa kufuata sheria za nchi.