SOKA: Elimu ya ‘Degree’ yapingwa urais ZFF
2021-03-04 16:01:35| cri

Viongozi wa timu mbali mbali na wadau soka visiwani Zanzibar, wamesema kiwango cha elimu ya shahada ya kwanza kilichowekwa kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) si jambo sahihi. Viongozi hao wamesema elimu ya shahada ya kwanza (Degree) kwa mtu anayetaka kugombea nafasi hiyo, ni kikwazo kikubwa na itakuwa vigumu kupatikana mtu huyo ambaye atashughulia mpira kama inavyotakiwa. Wamesema kuongoza mpira sio lazima kuwa na kiwango hicho cha elimu kama ilivyoeleza katiba ya ZFF,lakini, suala muhimu la kuongoza mpira lazima uwe na uzoefu katika masuala ya michezo na sio kuangalia ukubwa wa elimu.