Kenya yaahidi kuhimiza amani na ushirikiano wa kikanda wakati wa janga la COVID-19
2021-03-05 09:14:17| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliongea na mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo nchini Kenya, na kuwaambia kuwa kuna maendeleo mazuri nchini Sudan na Sudan Kusini, ambako mchakato wa amani unaendelea, na serikali ya Kenya itaendelea kutoa mchango wa uongozi kwenye kuhimiza amani na usalama.

Akiongea kwenye mkutano wa mwaka na mabalozi hao, Rais Kenyatta amesema Kenya itaendelea kuwa makini kwenye kutekeleza wajibu wake kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Shirika la maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD, pamoja na soko la pamoja na nchi za mashariki na kusini mwa Afrika COMESA.

Rais Kenyatta pia amekumbusha kuwa migogoro ya mipaka, uvamizi wa nzige, mabadiliko ya tabia nchi, COVID-19 na ugaidi, ni baadhi ya mambo yaliyofanya hali ya kibinadamu kwenye eneo la Afrika Mashariki iwe ngumu. Amesema Kenya itaendelea kushirikiana na nchi wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuhakikisha baraza hilo linatekeleza kazi zake kwa njia shirikishi, yenye mwitikio na majadiliano.