Wahamiaji 20 wafa maji pwani ya Djibouti
2021-03-05 09:42:34| CRI

 

 

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema wahamiaji wasiopungua 20 wa Afrika wamefariki katika pwani ya Djibouti.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo inasema watu wasiopungua 20 wamekufa maji baada ya wafanya magendo kuwatosa baharini mapema asubuhi ya Jumatano wakiwa kwenye safari yao ya kwenda Yemen kutoka Djibouti.

Taarifa hiyo inasema wahamiaji wasiopungua 200 wakiwemo watoto, walikuwa wamejaa ndani ya meli hii wakati ilipofunga safari, lakini wafanya magendo waliwatosa takriban watu 80 baharini baada ya dakika 30. Hadi sasa waokoaji wamepata miili ya wahanga 20.