Wakuu wa majeshi ya Somalia na Umoja wa Afrika watembelea vikosi ili kupanga operesheni za pamoja
2021-03-05 09:28:25| CRI

 

 

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), umesema kamanda wa vikosi vyake Bw. Diomede Ndegeya na mkuu wa jeshi la ulinzi la Somalia Bw. Odowaa Yusuf Rageh wametembelea vikosi vya Uganda kwenye mkoa wa kusini, ikiwa sehemu ya juhudi za kupanga operesheni za pamoja dhidi ya kundi la al-Shabaab.

Bw. Ndegeya amevipongeza vikosi vya Uganda kwa mchango wao katika kurudisha usalama na utulivu kwa kupambana na kundi la al-Shabaab na kupata uunganji mkono wa watu wa Somalia.

Kutokana na Mpango wa mpito wa Somalia, tume ya AMISOM itakabidhi majukumu ya kulinda usalama kwa jeshi la Somalia hatua kwa hatua na kuondoka nchini humo mwaka huu.