China ina imani na nia ya kutimiza lengo la asilimia 6 ya ongezeko la GDP
2021-03-05 18:20:13| CRI

China ina imani na nia ya kutimiza lengo la asilimia 6 ya ongezeko la GDP_fororder_8b13632762d0f703109b1868c7fa74352697c566

Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. He Lifeng leo amesema, kutokana na  takwimu za mwezi Januari na Februari, uchumi wa China umedumisha mwelekeo mzuri wa utulivu, na China ina imani na nia ya kutimiza lengo la ongezeko la GDP la asilimia 6.

Bw. He amesema, ongezeko la uuzaji bidhaa kwa nchi za nje katika mwezi Januari limezidi asilimia 50, kiwango cha PMI kimedumisha zaidi ya asilimia 50, matumizi ya umeme na uzalishaji wa umeme pia yameongezeka kwa asilimia 20. Hayo yote yameonyesha kuongezeka kwa uwezo wa kampuni za China kuzoea mabadiliko, hivyo China ina imani, nia, na uwezo wa kutimiza lengo la mwaka huu.