Watu kumi wafariki baada ya helikopta ya kijeshi ya Uturuki kuanguka
2021-03-05 08:59:10| CRI

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema helikopta moja ya jeshi la Uturuki ilianguka jana Alhamisi mashariki mwa nchi hiyo, na kusababisha vifo vya askari kumi na wengine watatu kujeruhiwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo, ajali hiyo ilitokea saa nane na dakika 25 alasiri, kazi ya utafutaji na uokoaji ilianza mara moja baada ya kutokea kwa ajali hiyo, na majeruhi wamekimbizwa hospitali.