SOKA: Serengeti Boys safarini Morocco
2021-03-05 16:16:46| cri

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limetoa orodha ya wachezaji 22 wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ watakaosafairi kuelekea Morocco kwa ajili ya fainali za Afrika z vijana (AFCON U17). Tanzania itawakilishwa na Serengeti Boys kwenye fainali hizo zitakazoanza Machi 13 hadi 31 katika viwanja vya El Bachir, Moulay Hassan na Père Jégo. Tanzania imepangwa Kundi B na itaanza kusaka ubingwa wa fainali hizo kwa kucheza dhidi ya Nigeria Machi 14, mchezo wa pili itacheza dhidi ya Algeria Machi 17 na itamaliza hatua ya makundi kwa kupapatuana na Congo Brazzaville Machi 20.