NDONDI: Ngumi wahitaji mashindano ya majaribio ya kimataifa
2021-03-05 16:17:43| cri

Kocha wa timu ya Taifa ya ngumi za Ridhaa Tanzania, Hassan Mzonge, amesema wanahitaji mashindano mawili ya kimataifa ya majaribio ili kukiimarisha kikosi kiwe cha ushindani kwenye mashindano yajayo. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kusaka tiketi ya kufuzu michezo ya Olimpiki ambayo imepangwa kuanza Julai mwaka huu Tokyo nchini Japan. Mzonge, amesema mashindano hayo yatasaidia kubaini kasoro na kuzifanyia kazi ili kukiweka tayari kikosi kimashindano. Amesema kuwa tayari timu imeshiriki mashindano ya majaribio yaliyoshirikisha mabondia kutokaZimbabwe ambayo yalimalizika Jumanne ya wiki hii yamewaza kusaidia kutambua kasoro sasa zinakwenda kufanyika maboresho.