Halmashauri zatakiwa kuvisajili vikundi vya kijamii Tanzania
2021-03-05 18:58:02| cri

Benki kuu ya Tanzania (BoT) imezitaka halmashauri zote nchini humo kusajili vikundi vyote vya kijamii vya huduma ndogo ya fedha ili vianze kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Benki kuu Tawi la Mbeya, Ibrahim Malogoi, wakati wa mafunzo ya mfumo maalum wa kusajili vikundi vya kijamii vya huduma ndogo ya fedha yanayotolewa kwa siku tatu kwa maofisa maendeleo wa halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.

Malogoi alisema kuwa Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka imeandaa miongozo na mifumo ya usajili wa vikundi vya kijamii na huduma za kifedha.

Alisema kwa mujibu wa ratiba inapaswa vikundi vyote vya kijamii viwe vimesajiliwa ifikapo Aprili 30, mwaka huu.