Mkutano wa Bunge la Umma la China wafunguliwa Beijing
2021-03-05 09:41:55| CRI

Mkutano wa Bunge la Umma la China wafunguliwa Beijing_fororder_1127170764_16149093881851n

Mkutano wa nne wa awamu ya 13 ya Bunge la Umma la China umefunguliwa leo Ijumaa hapa Beijing, na kuhudhuriwa na viongozi wa China akiwemo rais Xi Jinping, na wajumbe wapatao 3,000 wa bunge hilo.

Kwa mujibu wa ajenda, mkutano huo utasikiliza na kujadili ripoti ya kazi za serikali, mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano, na mswada wa mwongozo wa malengo ya mwaka 2035, ili kuweka mwelekeo na njia ya maendeleo ya China katika siku zijazo.

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa ripoti kuhusu kazi ya serikali, akijumuisha mafanikio ya maendeleo ya uchumi na jamii, na kueleza malengo na majukumu ya China katika miaka mitano ijayo.