FAO:Bei ya chakula duniani yaongezeka kwa miezi 9 mfululizo
2021-03-05 09:27:52| CRI

 

 

Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) imeonesha kuwa, bei ya chakula duniani kwa mwezi Februari iliendelea kuongezeka kwa mwezi wa 9 mfululizo, hasa bei za sukari na mafuta ya mimea zimeongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi.

FAO siku hiyo imeongeza makadirio ya uzalishaji wa nafaka duniani kwa mwaka 2020 hadi tani milioni 276.1, ikiwa ni ongezeko la 1.9 kuliko mwaka 2019, pia imekadiria kuwa uzalishaji wa ngano duniani kwa mwaka 2021 utaongezeka kwa miaka mitatu mfululizo, na kuweka rekodi mpya ya tani milioni 780.