Sudan Kusini yakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula baada ya mavuno kupungua kwa nusu
2021-03-05 09:13:13| CRI

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC) imetahadharisha kuwa watu wa Sudan Kusini wanakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na kupungua kwa mavuno ya mwaka jana.

ICRC imesema kwenye uchambuzi wake wa hivi karibuni kuwa mwaka jana jamii kwenye majimbo 9 kati ya 10 zimevuna chini ya asilimia 50 ya nafaka na mboga, ikilinganishwa na mwaka juzi.

Mkurugenzi wa ICRC Bw. Roberto Mardini amesema changamoto za hali ya hewa, pamoja na kuendelea kwa mgogoro na mapambano ya kutumia silaha, inafanya iwe vigumu kuwepo kwa mpito wa jamii kutoka kutegemea msaada wa chakula, na kujitegemea kwa uzalishaji wa chakula.  

Amesema wakati msimu wa mavuno unaanza makumi kwa maelfu ya familia hasa katika majimbo ya Jonglei, Upper Nile, Warrap, Unity na Lakes, wanahangaika kutokana na kutokuwa na mavuno ya kutoka msimu uliopita.