Polisi Morocco wakamata tani 4.06 za bidhaa za bangi
2021-03-05 08:59:34| CRI

Idara ya usalama wa taifa ya Morocco ilitoa taarifa jana ikitangaza kuwa polisi nchini humo walikamata tani 4.06 za bidhaa za bangi juzi Jumatano mjini Assilah, kaskazini mwa nchi hiyo, na idara za sheria nchini humo zimeanza uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo.