Kampuni ya China yawekeza dola milioni 110 katika uzalishaji wa vigae vya kauri na nepi za watoto nchini Zambia
2021-03-05 08:59:59| CRI

Kampuni ya Sunda ya China imeanza ujenzi wa viwanda viwili vya kuzalisha vigae vya kauri na nepi za watoto nchini Zambia.

Viwanda hivyo viwili vinajengwa kwenye Eneo la Viwanda la Kusini mwa Lusaka kwa uwekezaji na dola za kimarekani 110 kwa ujumla.

Hatua hiyo imekuja baada ya konseli kuu ya Zambia mjini Guangzhou kufanya mkutano na ujumbe kutoka kampuni hiyo.

Naibu mkuu wa kampuni hiyo Daniel Wang amesema mradi huu utatoa ajira 500 kwenye kipindi cha ujenzi na nafasi 1,500 za ajira baada ya uzalishaji kuanza rasmi.