Mahakama kuu ya Ghana yathibitisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020
2021-03-05 09:37:01| CRI

Mahakama kuu ya Ghana imetangaza kutupilia mbali madai ya rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020, na kuthibitisha uhalali wa matokeo hayo.

Mahakama imesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaoweza kuthibitisha matokeo ya uchaguzi huo si ya haki, na kufuta madai hayo.

Ghana ilifanya uchaguzi wa urais tarehe 7 mwezi Desemba mwaka jana. Tarehe 9 mwezi huo tume ya uchaguzi ya Ghana ilimtangaza mgombea wa chama tawala ambaye pia ni rais wa sasa Bw. Nana Akufo-Addo kuwa mshindi, na aliapishwa kuwa rais wa Ghana mwezi Januari mwaka huu.