Mtaalamu wa WHO asema “pasipoti ya Corona” haipendekezwi lakini labda haiepukiki
2021-03-05 09:13:47| CRI

Mkurugenzi wa Shirika la afya duniani WHO kanda ya Ulaya Bw. Hans Kluge ametaka nchi za eneo hilo kufuata kanuni za msingi kwenye mapambano dhidi ya janga ya COVID-19, wakati nchi hizo sasa zinashuhudia ongezeko la maambukizi.

Wakati maambukizi mapya yakiwa yameongezeka kwa asilimia 9 na kuwa zaidi ya milioni moja, hali ya wiki sita ya kupungua kwa maambukzi hayo imekatishwa, na aina mpya za virusi vya Corona zimeanza kuonekana kwenye eneo la Ulaya.

Ofisa hiyo pia amesema haungi mkono kuanzishwa ya “pasipoti ya Corona” ambayo nchi nyingi za Ulaya zimekuwa zikiizungumzia. Amesema WHO haipendekezi kuwepo kwa pasipoti hiyo, lakini pia anajua kwa kiasi fulani haiepukiki. Amesema japokuwa ni wazi chanjo inatoa kinga, lakini haijulikani chanjo inaweza kutoa kinga kwa muda gani, lakini haina maana pia kuwa inazuia kuenea kwa ugonjwa huo.