Kampuni nyingi Kenya zaendelea kupunguza mishahara ya wafanya kazi
2021-03-05 18:57:13| cri

Kampuni za kibinafsi zimeendelea kupunguza mishahara ya wafanyakazi wake kutokana na kudorora kwa biashara.Kampuni nyingi zimesema ziliamua kuchukua hatua hiyo ili kutowaachisha kazi wafanya kazi kutokana na kuathiriwa kwa biashara kutokana na janga la corona. Hata hivyo tangu kufunguliwa kwa uchumi kampuni nyingi zimesema zinategemea hali kurudi kawaida miezi michache ijayo. Janga la corona lilipunguza shughuli za biashara kwa asilimia 5.5 nchini Kenya kufuatia masharti ya usafiri na kufungwa kwa uchumi kutoka mwezi wa Aprili. Tangu wakati huo, kampuni nyingi za kibinafsi hazijafanikiwa kurudi katika hali ya kawaida.