Mji wa Dodoma waondoa masharti magumu ya kibiashara
2021-03-05 18:56:51| cri

Halmashauri ya mji wa Dodoma imeondoa masharti magumu ya kibiashara katika Soko Kuu la Job Ndugai ikiwamo kupunguza bei ya vizimba.

Kwa sasa bei ya vizimba hivyo ni kati ya Sh. 25,000 hadi 30,000, uamuzi huo unalenga kuwavutia zaidi wafanyabiashara.

Hatua hiyo imetokana na kudorora kwa biashara kwenye eneo hilo huku baadhi ya vizimba vikikosa wafanyabiashara.

Mkurugenzi wa Jiji hilo, Joseph Mafuru amesema soko hilo lina vizimba 365. Kati yake, 303 ndivyo vimetolewa kwa watu huku maeneo ya vibanda ghorofa ya kwanza ni 175 na yaliyotolewa ni 153.

Alisema migahawa mikubwa miwili, machinjio ya kuku na vibanda vinane vya kushushia mizigo bado havina watu.

Wafanya biashara waliokuwa Nanenane na kwenye kituo cha mabasi yanayofanya safari zake ndani ya Dodoma wamehamishwa hadi kwenye soko hilo.