China yakaribisha wageni kutembelea Xinjiang
2021-04-02 19:35:47| CRI

China yakaribisha wageni kutembelea Xinjiang_fororder_VCG111320417519

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amefahamisha hali ya katibu mkuu wa SCO Vladimir Imamovich Norov na mabalozi wa nchi mbalimbali walipotembelea Xinjiang.

Amesema China inakaribisha wageni kutembelea Xinjiang na kushuhudia mandhari nzuri ya Xinjiang, maisha mazuri ya watu wa Xinjiang na maendeleo ya uchumi ya Xinjiang. Amesema China inaamini kuwa, uvumi hukomeshwa na mwenye busara, na haki iko mioyoni.

Amesema baada ya ziara hiyo, wameshuhudia ukweli wa utulivu wa jamii, masikilizano kati ya makabila tofauti na dini tofauti, na maendeleo madhubuti ya kiuchumi. Wameeleza nia yao ya kuhimiza ushirikiano kati ya nchi zao na Xinjiang, China, hasa katika mapambano dhidi ya ugaidi na sekta ya uchumi na biashara.