Kenya kudhibiti uvamizi wa nzige wa jangwani ifikapo katikati ya Aprili
2021-04-02 08:49:59| CRI

Kenya jana ilitangaza kuwa uvamizi wa nzige wa jangwani utadhibitiwa kikamilifu ifikapo katikati ya Aprili.

Akiongea na wanahabari mjini Nairobi, msemaji wa serikali Cyrus Oguna amesema juhudi za kudhibiti na kuzuia zinazofanywa na serikali kuu ikishirikiana na serikali za kaunti pamoja na washirika wengine wa kimaendeleo kama vile Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani la Afrika Mashariki DLCEO na Benki ya Dunia, wameweza kupunguza makundi ya nzige hadi matatu na kusisitiza kwamba juhudi zinaendelea kufanywa ili kudhibiti kundi la mwisho.

Bw. Oguna amebainisha kuwa jumla ya kaunti 25 zimevamiwa na wadudu hao kwa kiwango tofauti na sasa kuna maendeleo makubwa yaliyofikiwa ya kuwadhibiti.