ZANZIBAR: NAKISI YA BIASHARA YAONGEZEKA
2021-04-05 18:14:29| cri

 

Thamani ya biashara kwa mwezi Februari 2021, imeonyesha nakisi ya shilingi bilioni 86.8, nakisi ambayo imeongezeka kwa asilimia 37.8 ikilinganishwa na mwezi Januari.

Hayo yamebainishwa wakati wa uwasilishaji wa takwimu za biashara za kimataifa kwa mwezi Februari katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Mazizini mjini Unguja mwishoni mwa wiki jana.

Mkuu wa Kitengo cha Utoaji wa Huduma, Bakar Khamis Kondo, alisema, ikilinganishwa na mwezi Februari 2020, nakisi hiyo imeongezeka kwa asilimia 47.8.

Alisema, bidhaa zilizosafirishwa nje ya taifa, zilifikia shilingi milioni 4,176.4 huku zikipungua  kwa asilimia 74.5% ikilinganisha na mwezi Februari 2020 na imeongezeka kwa aslimia 100 ikilinganisha na mwezi Januari 2021.

Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Ulrick Mumburi, alisema, ipo haja ya kuongezewa thamani kwa bidhaa zinazosafirishwa nje ili kuongeza mapato ya fedha za kigeni.