SOKA: Tanzania yafuzu AFCON ya ufukweni
2021-04-05 16:44:03| cri

Timu ya taifa ya soka ya ufukweni ya Tanzania imefuzu fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayofanyika nchini Senegal licha ya kufungwa 6-4 na Burundi katika mchezo wa marudioano uliochezwa kwenye fukwe za Coco jijini Dar es Salaam jumamosi. Katika mchezo huo ambao Tanzania walikuwa wenyeji, imefuzu kwa jumla ya mabao 12 – 9 baada ya ushindi wa bao 8 – 3 waliopata katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika fukwe hizo kutokana na Burundi kuomba mechi zake zichezwe Tanzania kwa kuwa uwanja wao umejaa maji.