Bibi mwenye miaka 80 ashindwa kutibiwa baada ya kujeruhiwa mguu kutokana na watoto wake kutotaka kumgharamia
2021-04-07 15:40:30| Cri

Bibi mwenye umri wa miaka 80 mkoani Shandong, alianguka mlangoni mwa nyumba yake na kujeruhiwa mguu, baada ya kukaguliwa hospitalini aligunduliwa kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji.

 

Baada ya kupata habari hii, watoto saba wa bibi huyo walikwenda hospitalini. Lakini badala ya kumshughulikia, walimrudisha nyumbani, kwani hawakuwa na mpango wa kulipa gharama kwa ajili ya mama yao kufanyiwa upasuaji.

 

Hivi sasa bibi huyo analala nyumbani, huku mguu wake ukiwa bado unauma vibaya. Bibi huyo alisema kwa huzuni kubwa ana watoto saba ambao wanne ni wakiume na wengine watatu ni wa kike, lakini hawapendi kunigharimia matibabu, na hakuna hata mmoja aliyempatia chakula au maji, analoweza kufanya ni kusubiri kufa.

 

Jamaa wa bibi huyo walisema daktari amewaambia kuwa ikiwa mzee hatatibiwa atalemaa siku za baadaye.