Je! Unajua miiko ya kupeana zawadi nchini China?
2021-04-07 15:41:01| Cri

China ni nchi kubwa yenye mila na desturi, pia ina miiko mingi ya jadi na ya kisasa, ambayo inahusiana na maisha ya watu. Je, unajua miiko ya China wakati wa kuzawadia watu?

 

  1. Usizawadie watu saa, kwa sababu tamshi la “saa” ni sawa na “mwisho”, na kuzawadia watu “saa” kunamaanisha kuwatakia watu “kufariki”. Na saa ya mkono ni aina mojawapo ya saa hizo, pia haifai kuzawadia watu. Lakini ikiwa unataka kumnunulia mtu saa ya mkono, unaweza kumtaka anunue, kisha umlipie.

 

  1. Usizawadie watu viatu, kwani tamshi la “viatu” ni sawa na “uchawi“Bewitched kwa hivyo ukizawadia watu viatu (isipokuwa familia inaponunulia wanafamilia wengine viatu), inamaanisha kuwafanyia uchawi, na itaweza kuharibu uhusiano wenu.

 

  1. Usizawadie watu mwavuli, kwa sababu “mwavuli” ni sawa na “kutawanyika”, hivyo ni bora kutozawadia marafiki mwavuli, ambayo inamaanisha kuwa mtatengana baadaye. Pia usizawadie watu pea au maboga, matunda haya mawili vilevile yanamaanisha kutamani wengine watengane.

 

  1. Usizawadie watu mishumaa, kwa sababu kwa mujibu wa mila na desturi za kichina, mishumaa inatumiwa kutoa heshima kwa watu waliofariki, kwa hivyo ni mwiko kuwazawadia wengine.

 

  1. Usizawadie watu wanaserere au mawe ambayo chanzo chake hakijulikani, kwani baadhi ya watu wanaona kuwa wanaserere na mawe ambayo chanzo hakijulikani vitaleta bahati mbaya, lakini haihusiani na kuwazawadia watoto wa jamaa au rafiki.