Mtaalamu wa Ethiopia aitaka jumuiya ya kimataifa izuie kuongezeka kwa “utaifa wa chanjo”
2021-04-08 08:57:59| cri

 

 

Mtaalamu wa masuala ya sera za Umma kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia Profesa Costantinos Constatinos, ameitaka jumuiya ya kimataifa izuie kuongezeka kwa “utaifa wa chanjo”, na kuhakikisha usambazaji wa chanjo ya COVID-19kwa usawa.

Prof. Costantinos amesema, ni muhimu sana kueneza upatikanaji wa chanjo dunia kote, kwa sababu kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona katika nchi fulani hakuwezi kuifanya dunia iwe salama.

Bw. Costantinos amesema, baadhi ya nchi zilizoendelea zimehifadhi idadi kubwa ya chanjo inayozidi mahitaji yao, na kusababisha kuongezeka kwa “utaifa wa chanjo”.

Amezitaka nchi zilizoendelea zifanye juhudi kushiriki kwenye uhakikishaji wa kusambaza chanjo ya COVID-19 kwa njia ya usawa duniani.