Bei ya petroli ,dizeli na mafuta taa yaongezeka Tanzania
2021-04-08 17:09:13| cri

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini Tanzania (EWURA) imetangaza ongezeko la bei za mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa yanayoingia nchini humo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na EWURA ,bei za rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli zimeongezeka kwa Sh142 na Sh85 kwa lita huku bei ya jumla ikiongezeka kwa Sh141.92 na Sh84.95 kwa lita,mtawalia.

Ongezeko la bei hizo linamaanisha kuwa sasa wakazi wa Dar es salaam watanunua lita moja ya petroli kwa Sh2,123 na dizeli kwa Sh1,996 kutoka Sh1,981 na Sh1,911 waliyokuwa wakinunua mwezi uliopita.

Mabadiliko hayo ya bei ya mafuta kwa wanunuzi wa jumla na rejareja yaliyoanza kutumika jana , yametokana na ongezeko la bei ya mafuta katika soko la dunia na gharama ya usafirishaji.