China yatoa mwongozo wa kufungua zaidi soko katika bandari ya biashara huria ya Hainan
2021-04-08 18:23:43| Cri

China imetoa mwongozo unaounga mkono kufungua zaidi soko katika bandari ya biashara huria ya Hainan, ikiwa ni juhudi mpya za kukijenga kisiwa hicho kuwa bandari ya ngazi ya juu na yenye ushawishi mkubwa duniani.

Mwongozo huo uliotolewa leo kwa pamoja na Tume ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi na Wizara ya Biashara, imefafanua hatua za uvumbuzi wa soko katika sekta za madawa na afya, kuboresha uingizaji wa fedha katika soko na kuendeleza mazingira, pia kukufungua zaidi sekta za utamaduni na elimu.

Mwongozo huo umesema, China itaunga mkono maendeleo ya uvumbuzi wa vifaa vya afya huko Hainan, na pia kuboresha mauzo ya dawa zinazoagizwa na madaktari kupitia mtandao.