Benki ya Dunia yasema mustakbali wa kazi Afrika unategemea ukuaji wa kidijitali
2021-04-08 17:08:48| cri

Sera ambazo zinakuza uwekezaji katika uvumbuzi na teknolojia zinaweza kusaidia kuweka upya miundo ya uchumi na kuwezesha bara la Afrika kwenda sambamba na ulimwengu wote.

Hayo ni kwa mujibu wa Ripoti ya uchambuzi wa mara mbili kwa mwaka wa Benki ya Dunia kuhusu uchumi wa Afrika.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa teknolojia za dijitali zinatoa fursa ya vyanzo vingi vya uchumi wa Afrika mbali na vyanzo vya asili , kwa kusaidia kupunguza shida za kifedha zinazokabiliwa na wajasiriamali.

Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia barani Afrika,Abert G.Zeufack,amesema mageuzi kabambe ambayo yanasaidia kuunda kazi,kuimarisha ukuaji sawa,kulinda walio hatarini na kuchangia uendelevu wa mazingira yatakuwa ufunguo wa kuimarisha juhudi za ukuaji kwenda mbele kupata ahueni zaidi katika bara la Afrika.

Ukuaji barani Afrika sasa unatabiriwa kuongezeka kati ya asilimia 2.3 na 3.4 mnamo 2021,kulingana na sera zilizopitishwa na nchi na jamii ya kimataifa.