SOKA: Ulimwengu: TP Mazembe itakaa sawa
2021-04-08 18:27:36| cri

Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo,Thomasi Ulimwengu amesema kufanya vibaya kwa klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa msimu huu ni upepo mbovu, na anaamini kuwa msimu ujao mambo yatakuwa mazuri. Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, TP Mazembe, wakiwa katika kundi B wanashika nafasi ya mwisho nyuma ya timu za Mamelod Sundowns, CR Belouizdad na Al Hilal. Ulimwengu anasema, katika mpira wa miguu timu, kubwa nyingi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri kama ilivyozoeleka huteleza na kupitia upepo mbaya, jambo ambalo anaamini halitajitokeza tena katika msimu ujao wa ligi hiyo.