Waziri mawasiliano na uchukuzi Zanzibar afurahishwa na kasi ya uondoshwaji wa makontena katika bandari kuu ya Zanzibar
2021-04-22 19:21:48| cri

Waziri mawasiliano na uchukuzi Zanzibar , Mhe Rahma Kassim Ali amefurahishwa na kasi ya uondoshwaji wa makontena katika bandari kuu ya Zanzibar na kumtaka mkurugenzi wa bandari Bw. Nahat Mohammed Mahfoudh kuendelea na kasi hiyo ili kuongeza mapato ya Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa bandari amesema ili kuendena na kasi ya maendeleo iliyopo ipo haja kwa mamlaka ya bandari kutumia mfumo mpya wa teknolojia wa utowaji mizigo badala ya mfumo wa zamani ili kurahisisha huduma kwa watumiaji wa banadari hiyo.

Wakati huo huo waziri wa mawasiliano na uchukuzi ametoa agizo kwa wakala wa barabara kuhakikisha wanaunda kamati itakayoshughulikia ukarabatiwa barabara zote zenye mashimo kwa kuanza na barabara ya uwanja wa ndege ambayo imekuwa ikileta taswira mbaya ya mji wa Zanzibar.

Sambamba na hilo alisisitiza wafanyakazi wa wakala wa barabara kupatiwa stahiki zao wanazostahiki ili wafanyakazi hao wafanye kazi kwa ufanisi..