Kenya yaripoti maendeleo ya njia ya kisayansi kuwaokoa faru weupe
2021-04-22 20:31:14| cri

Kenya yaripoti maendeleo ya njia ya kisayansi kuwaokoa faru weupe_fororder_VCG111236927154

Kenya imetangaza imefanikiwa kutungishwa mimba nne za faru weupe ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaokoa faru hao walio kwenye hatari ya kutoweka.

Mamlaka ya wanyamapori ya Kenya KWS na kundi la wanasayansi wa kimataifa walifanikiwa kufanya hivyo mwezi uliopita kwa kutumia mayai yaliyovunwa kutoka kwa faru wawili jike waliobaki wanaitwa Fatu.

Waziri wa utalii na wanyamapori wa Kenya Bw. Najib Balala amesema wamefurahishwa na matokeo hayo ya kimaabara, na kusema hatua ya pili ni kuweka mimba hizo kwa faru jike walioko kwenye kituo cha Ol-Pejeta.

Mimba hizo kwa sasa zitahifadhiwa pamoja na nyingine tano zilizotungishwa hapo awali zikisubiri hatua hiyo ya pili.