Baraza la seneti la bunge la Marekani lapitisha muswada wa kupambana na uhalifu dhidi ya Waasia
2021-04-23 19:23:09| cri

Baada ya kufika makubaliano kati ya vyama vya Democratic na Republican vya Marekani, baraza la seneti ya bunge la Marekani limepitisha muswada wa kupambana na uhalifu wa chuki dhidi ya Waasia kutokana na janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa muswada huo, wizara ya sheria ya Marekani itaanzisha idara mpya kuharakisha kushughulikia uhalifu dhidi ya Waasia, kuanzisha mfumo wenye lugha mbalimbali wa kuripoti uhalifu kwenye mtandao, kuzingatia zaidi mambo ya kuripoti, kufuata na kutoa mafunzo kuhusu uhalifu huo katika idara mbalimbali za sheria za majimbo na kuondoa maneno ya ubaguzi kwenye maelezo ya hali ya janga hilo. Habari zinasema muswada huo utapitishwa baada ya kuchunguzwa na baraza la wawakilishi la bunge la Marekani.