Mtaalam wa Afrika Kusini aonya Japan kutupa majitaka ya nyuklia baharini kutaleta maafa kwa dunia nzima
2021-04-23 18:36:23| CRI

Mtaalam wa Afrika Kusini aonya Japan kutupa majitaka ya nyuklia baharini kutaleta maafa kwa dunia nzima_fororder_微信截图_20210423201209

Mpango wa Japan kutupa majitaka ya nyuklia baharini unafuatiliwa na dunia nzima. Mtaalam wa mazingira ya asili wa Afrika Kusini Bibi Liz McDaid, anaona kitendo hicho kitaleta maafa kwa binadamu wa dunia nzima.

Bibi Liz amesema mionzi ya majitaka ya nyuklia itaathiri viumbe walio karibu na samaki wanaokula, kwa kuwa maji ya bahari yanasafiri, hivyo mionzi hiyo itaathiri bahari nzima. Ameonya kuwa samaki wengi watatoweka, na binadamu pia wataathiriwa.

Amesisitiza kuwa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Nishati ya Nyuklia cha Fukushima kilitoa umeme kwa Wajapani kwa miaka mingi, lakini watu wa nchi nyingine hawakunufaika na chochote. Ili kubana matumizi, Japan inataka kutupa majitaka ya nyuklia baharini, na kuleta maafa kwa dunia nzima, hili si jambo linalofaa.