The Kenya Airways and DR Congo national carrier have signed a partnership agreement
2021-04-23 18:38:49| cri

Mashirika ya ndege ya Kenya na Jamhuri ya Kongo yamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara kati yao. Makubaliano hayo ambayo yalisainiwa mbele viongozi wa nchi hizo mbili Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Kongo Felix Tshisekedi mjini Kinshasa yatahakikisha pande zote mbili zinashirikiana katika utoaji wa mafunzo, ukarabati wa pamoja wa ndege na kubadilishana abiria. Makubaliano hayo ya miaka miwili yanalenga kuimarisha mashirika hayo mawili ili yaweza kupata mafanikio ya kibiashara barani Afrika na nje ya bara hilo.Makubaliano hayo yalisainiwa na katibu mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Allan Kilavuka na mwenzake wa Kongo Desire Balazire Bantu.