Zaidi ya wahamiaji haramu 100 wafa maji kwenye pwani ya Libya
2021-04-23 19:30:32| CRI

 

 

Kiongozi mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM Bw. Eugenio Ambrosi amesema zaidi ya wahamiaji haramu 100 wamekufa maji kwenye ajali ya kuzama kwa boti kwenye pwani ya Libya.

Bw. Ambrosi amesema kwa njia ya Twitter kuwa watu hao wamekufa kwenye eneo la katikati ya Mediterranean, na hali hii imetokana na sera za binadamu ambazo zimeshindwa kufuata sheria ya kimataifa na mambo ya kimsingi ya binadamu. 

Libya kwa sasa imekuwa ni sehemu inayotumiwa zaidi na mamia ya wahamiaji haramu wanaotaka kwenda Ulaya. Mwaka jana zaidi ya watu elfu 11 waliokolewa na kurudishwa Libya, na 318 walikufa na wenye 597 walipotea wakiwa njiani.